Muungano wa Azimio kutoa mwelekeo wake mpya siku ya ijumaa

  • | K24 Video
    224 views

    Muungano wa Azimio sasa utatoa mwelekeo wake mpya siku ya ijumaa katika mkutano wa hadhara utakaokuwa eneo la Kibra baada ya mazungumzo kugonga mwamba. Mkutano huo utafanyika pindi tu kinara wa Azimio Raila Odinga atakaporejea kutoka ughaibuni. Muungano huo vile vile umetoa ilani kwa polisi kuhusu maandamano yao ya Jumanne wanayopania kuyafanya katikati mwa jiji na kuwasilisha malalamishi yao katika afisi za rais zilizoko katika barabara ya harambe.