Muungano wa Kenya Kwanza umekosoa Azimio la umoja kwa kususia mazungumzo

  • | K24 Video
    102 views

    Muungano wa Kenya Kwanza umekosoa Azimio la umoja kwa kususia mazungumzo ya kutafuta maridhiano kati ya serikali na upinzani. Mwenyekiti George Murugara amesema upande wa serikali uko tayari kuendelea na mazungumzo hayo wakati wowote. Muungano wa Azimio umetangaza kikao cha wabunge wake jumanne wiki ijayo ili kutoa mwelekeo mpya. Wakati huohuo kamati ya ushirikiano ya vyama vya kisiasa nchini, PPLC, imemtetea msajili wa vyama vya siasa Ann Nderitu kuhusiana na utata unaozunguka cha Jubilee ambao ni mojawapo ya maswala yaliyosababisha mazungumzo yasitishwe.