Muungano wa wafanyikazi wadai malipo ya zaidi ya wafanyikazi 150 walioajiriwa na kampuni ya Meta

  • | Citizen TV
    157 views

    Muungano wa wafanyikazi katika sekta ya mawasiliano sasa imetoa wito kwa wizara ya Leba, kuingilia kati na kufanikisha malipo ya mishahara kwa raia zaidi ya 150 wa kigeni walioajiriwa na kampuni ya Meta inayomiliki mtandao wa Facebook. Akizungumza jijini Kisumu, katibu wa muungano huo Benson Okwaro anasema kuwa wafanyikazi hao wameshindwa kujikimu baada ya kampuni ya Meta kusitisha kandarasi zao za uajiri mwezi Aprili. Mahakama ya juu nchini ilitoa amri tarehe 11 mwezi Mei, ikiitaka kampuni ya Meta kuendelea kuwalipa wafanyikazi hao mishahara.