Skip to main content
Skip to main content

Mvua kubwa na upepo mkali wasababisha uharibifu Kisumu

  • | Citizen TV
    37,972 views
    Duration: 1:27
    Mali ya thamani isiyojulikana iliharibiwa jijini Kisumu kufuatia upepo mkali na mvua kubwa iliyoanza ghafla Alhamisi jioni. Magari kadhaa yaliangukiwa na miti na mabango, huku kuta zikibomolewa na nyaya za stima kukatika kutokana na upepo huo. Msimamizi wa Jiji la Kisumu, aliyezungumza baada ya kukagua uharibifu huo, alisema serikali ya kaunti inashirikiana na asasi mbalimbali kufungua mabomba na mitaro ya majitaka ili kuzuia mafuriko. Idara ya utabiri wa hali ya anga ilibashiri kuanza kwa msimu wa mvua katika ukanda wa magharibi wiki hii, huku mvua hizo zikitarajiwa kuongezeka kutokana na El Niño.