Mwaka mmoja wa Rais Ruto mamlakani

  • | K24 Video
    45 views

    Tume ya kutetea haki za binadamu, khrc imesema ufisadi unasalia donda sugu katika serikali ya Rais William Ruto. Katika taarifa yao kuhusu mwaka mmoja wa serikali ya Kenya Kwanza, tume hiyo inasema serikali ya Rais Ruto inaendelea kuhitilafiana na kesi za ufisadi, taasisi na tume huru nchini, kubagua wakenya na polisi kutumia nguvu kupita kiasi. Rais Ruto pia amelaumiwa kwa kuhujumu demokrasia kwa kuingilia vyama vingine.