- 239 viewsGharama ya juu ya matibabu ya ugonjwa wa figo imemfanya Mwalimu mmoja mwenye umri wa miaka 34 kutoka Diani, Kaunti ya Kwale, kujipata kwenye njia panda. Maisha ya mwalimu huyo yalibadilika baada ya mkono wake wa kulia kupooza kufuatia hitilafu wakati wa matibabu ya kusafisha damu. Sasa mwalimu huyo ameshindwa kuendelea na kazi yake huku gharama ya juu ya upandikizaji wa figo ikimshinda.