Mwanablogu Ndiangui Kinyagia atekwa nyara

  • | Citizen TV
    8,123 views

    Familia moja eneo la kitengela jioni hii inamtafuta mwana wao, mwanablogu ndiangui kinyagia aliyetoweka baada ya maafisa wa upelelezi kudaiwa kumchukua nyumbani kwake jumamosi. Kwenye tukio hili, maafisa hao wanaripotiwa kuchukua vipakatalishi, simu na pasipoti zake. Familia inasema kinyagia alikuwa akiishi kwa hofu baada ya kushuku kuna watu wanaomfuata kufuatia taarifa alizochapisha kwenye mtandao wa X.