Mwanafunzi Agnes Muthoni aliyepata alama ya 373 kwenye mtihani wa KCPE alipiwa karo Isinya, Kajiado

  • | Citizen TV
    1,008 views

    Mwanafunzi Agnes Muthoni Kutoka Isinya Kaunti ya Kajiado ambaye alikuwa amepoteza matumani ya kuendelea na elimu baada ya kukosa karo ya kumwezesha kujiunga na shule ya upili ya Nyabururu hatimaye amefanikiwa kuingia darasani Katika shule ya wasichana ya Kitaifa ya Moi Girls Isinya. Muthoni ambaye alipata alama ya 373 kwenye mtihani wa KCPE Mwaka uliopita amelipiwa karo na mhisani baada ya kisa chake kuangaziwa na Runinga ya citizen wiki iliyopita.