Mwanafunzi anayeugua anahofia kutofanya mtihani wake

  • | Citizen TV
    Mwanafunzi mmoja wa kidato cha nne katika shule ya upili ya ESHITSITSWI, ENEO BUNGE LA BUTERE, KAKAMEGA huenda akakosa kufanya mtihani wa kcse kutokana na mzigo wa maradhi ya figo. Mwanafunzi huyo amekuwa akiugua tangu mwaka 2019 na anahitaji shilingi milioni mbili za matibabu. Amekuwa akienda kliniki mara mbili kwa wiki mjini kisumu baada ya kushindwa kugharamia kupandikizwa figo nyingine. Walimu wa shule hiyo wamekuwa wakichanga pesa kumsaidia kusafiri hadi kisumu kusafishwa figo ila mzigo huo sasa unawalemea.