Mwanafunzi mmoja abuni mfano wa nyumba ambayo inayokunjwa na kuhamishwa

  • | Citizen TV
    644 views

    Mdahalo wa nyumba za bei nafuu umo midomoni mwa wakenya wengi, iwe kwa hiari au kwa sheria. Lakini vipi kuhusu mpango wa nyumba? Mwanafunzi mmoja katika taasisi ya teknolojia ya Siaya amebuni mfano wa nyumba ambao anaamini utasaidia watu ambao wanataka kuhama kutoka sehemu moja kwenda nyingine panapohitajika. Na jinsi mulindi carey anaripoti, vincentia ouko alichochewa na hali ya familia yake kuunda nyumba ya kuhamishwa ilipolazimishwa kukimbia nyumbani kwao kericho wakati wa machafuko ya baada ya uchaguzi wa 2007/08.