Mwanafunzi mzee zaidi Rwanda

  • | BBC Swahili
    711 views
    Akiwa na umri wa miaka 54, Rusengamihigo anabeba rekodi ya kuwa mwanafunzi mwenye umri mkubwa zaidi nchini Rwanda katika shule za msingi na sekondari. Bwana Jean Marie Vianney Rusengamihigo ni mwanafunzi wa mwaka wa tano katika shule ya msingi ya SHANGI katika Wilaya ya Nyamasheke Magharibi mwa Rwanda. Aliamua kurudi shuleni baada ya miaka 39, Lakini ni nini kilimfanya arudi shuleni? Mwandishi wa BBC Yves Bucyana alimtembelea na kuandaa taarifa hii. #bbcswahili #rwanda #elimu