Mwanahabari wa Mediamax Catherine Wanjeri apigwa risasi na polisi kaunti ya Nakuru

  • | K24 Video
    293 views

    Katika kile kilichoonekana kama matumizi ya nguvu kupita kiasi na polisi wakati wa maandamano ya leo, Catherine Wanjeri kariuki, mwanahabari wa Mediamax sasa anauguza majeraha ya risasi. Catherine alipigwa risasi mguuni alipokuwa akirekodi maandamano hayo katikati mwa mji wa Nakuru. wakati wa tukio hilo mwanahabari huyo alikuwa pamoja na mwenzake ambaye pia alijeruhiwa.