Mwanaharakati Boniface Mwangi aachiliwa kwa dhamana ya KSH. Milioni 1

  • | Citizen TV
    3,409 views

    Mwanaharakati Boniface Mwangi anasema kuna njama ya serikali ya kumuua kutokana na msimamo wake wa kutetea maswala yanayohusu vijana. Akizungumza katika mahakama ya Kahawa aliposhtakiwa kwa kupatikana na risasi na vitoa machozi bila leseni, mwanaharakati huyo aliapa kuendelea kuikosoa serikali haswa kuhusu mauaji ya waandamanaji.