- 15,866 viewsDuration: 28:10Mwanamfalme wa zamani na mdogo wa Mfalme Charles, Andrew Mountbatten-Windsor, amekamatwa na polisi wa Uingereza kwa tuhuma za utovu wa nidhamu katika ofisi ya umma. Polisi wanasema wanatathmini ripoti kwamba mwanamfalme huyo wa zamani alidaiwa kutoa habari za siri kwa Jeffrey Epstein ambaye alipatikana na hatia ya uhalifu wa kingono, tukio linalodaiwa kufanyika wakati Andrew alipokuwa mjumbe wa biashara wa Uingereza. Andrew Mountbatten Windsor amekana makosa yanayohusiana na nyaraka za Epstein. #AndrewMountbattenWindsor #Epstein #BBCSwahili Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw