Mwanamke afariki kufuatia mafuriko eneo la Gakungu Kirinyaga

  • | Citizen TV
    587 views

    Mtu mmoja ameaga dunia na mamia kusalia bila makao kufuatia mafuriko yanayoendelea sehemu mbalimbali nchini. Mwanamke wa miaka 60 na miwili alikufa maji baada ya kuzidiwa na mafuriko alipokuwa akivuka mto Thiba kaunti ya Kirinyaga. Haya yanajiri huku waathiriwa wa mafuriko ambao wameachwa bila makao sasa wakiirai serikali kuweka mikakati ya kudumu ili kuzuia mafuriko ya mara kwa mara.