Mwanamke amuua mshukiwa wa ubakaji eneo la Emgwen kaunti ya Nandi

  • | Citizen TV
    408 views

    Hali ya taharuki ilitanda katika kijiji cha Kolong kwenye eneo bunge la Emgwen kaunti ya Nandi baada ya wakazi wenye hamaki kumvamia mwanamke anayedaiwa kumuua mwanamume aliyepatikana akimnajisi bintiye wa miaka 2. Akidhibitisha kisa hicho OCPD wa Nandi ya kati David Anyir, alisema kuwa mama huyo alikiri kumuua mwanaume mmoja kwa kumkatakata alipompata mtu huyo akimnajisi bintiye nyumbani kwake.Anyir aliongeza kusema kuwa mama huyo alimwarifu chifu wa eneo la Kamobo kuwa wakazi walikuwa wanamwandama kufuatia mauaji hayo .