| MWANAMKE BOMBA | Amina Ramadhan - Polisi aliyemwokoa mama, mwanawe wakati wa kafyu

  • | Citizen TV
    Siku moja tu baada ya marufuku ya kutoka nje usiku kuanza kutekelezwa, picha yake ilisambaa mitandaoni wengi wakimtaja kama polisi muungwana. Hisani yake ya kumsaidia mwanamke aliyekuwa na mtoto na mikoba ikiionekana kuwa nadra miongoni mwa polisi ambao mara nyingi hunasibishwa na matukio ya kutumia nguvu kupita kiasi. Bila shaka wasiomjua,sasa wanahamu ya kumfahamu vyema pamoja na utendakazi wake na ndio maana nilimtafuta na kumvisha taji la mwanamke bomba wiki hii. #MwanamkeBomba​ #AminaRamadhan