| MWANAMKE BOMBA | Catherine Chacha - Muuguzi anayewasaidia waathiriwa ubakaji

  • | Citizen TV
    Suala la ubakaji limekuwa donda sugu katika maeneo mengi nchini huku waathiriwa wengi wakikosa haki kwa kutoripoti visa hivyo kutokana na uongo na kuchelea aibu. Hata hivyo, kuna muuguzi katika hospitali moja kaunti Migori ambaye yuko katika mstari wa mbele kuhakikisha kwamba waathiriwa wa ubakaji wanapata haki na wahusika wanachukuliwa hatua za kisheria. Mwanadada huyo mwenye umri wa miaka 34 amekuwa akifanya juhudi hizo bila malipo kando na majukumu yake ya uuguzi na ndiye tunayemvisha taji la Mwanamke Bomba wiki hii.