Mwanamke Bomba

  • | Citizen TV
    309 views

    Kazi za mikono mara nyingi katika jamii ya Maasai zimekuwa zikitengewa wanaume. Hata hivyo Maria Salash amekiuka dhana hiyo na kuanzisha kazi ya kuosha magari na pikipiki katika eneo la tinga, Oltepesi, huko Kajiado Magharibi. Maria anasema alichukua hatua hiyo ili kuikimu familia yake baada ya mumewe kufariki na ufugaji ambao ulikuwa tegemeo kuathirika na mabadiliko ya hali ya anga. Maria Salash ndiye anayetupambia makala ya leo ya Mwanamke Bomba.