Mwanamke Bomba | Dorcas Lolngojine anawahamasisha wafugaji Samburu

  • | Citizen TV
    1,274 views

    Swala la malisho ya mifugo kwa jamii za wafugaji kaskazini mwa nchi linazidi kuwatatiza tangu jadi. Kwenye makala ya wiki hii ya mwanamke bomba tunamuangazia dorcas lolngojine mwanamke aliyejitolea kuwahamasisha wafugaji kaunti ya samburu kupanda nyasi zinazostahimili kiangazi ili kujihakikishia malisho ya kutosha na kusuluhisha mizozo ya kijamii ya kila mara yanayosababishwa na uhaba wa malisho. Dorcas huendesha kampeni yake sehemu za malisho anakotangamana na wafugaji na wakati mwingine analazimika kupiga kambi na wafugaji malishoni kwa siku kadhaa akiendeleza kampeni hizo. Hii hapa simulizi yake.