MWANAMKE BOMBA | Roselane Ambasi alibobea kwenye sekta ya uhandisi

  • | Citizen TV
    1,090 views

    Katika miaka ya nyuma sekta ya uhandisi ilikuwa na idadi ndogo mno ya wanawake huku wachache waliofuzu wakipata fursa nzuri ya kuajiriwa katika mashirika mbalimbali. Shirika la Kenya Pipeline ni miongoni mwa yale yaliyotoa fursa kwa wanawake kuendeleza taaluma zao, na Roselane Ambasi ni miongoni mwa wachache waliopata fursa ya ajira miaka ya 90. Licha ya kumpoteza mumewe na kuachwa na malezi wa watoto wadogo watatu Roselane hakuyumbishwa na changamoto zilizomkabili bali alijizatiti na kubobea kazini kiasi cha kupanda ngazi kufikia kiwango ambacho hata wanaume wengi wanakimezea mate. Hii leo ndiye anayetupambia makala ya Mwanamke Bomba, shirika hilo likiadhimisha miaka 50 tangu lianze shughuli zake.