Mwanamke Bomba |Rukiya Mohamed hutangamana na nyoka kila siku

  • | Citizen TV
    8,219 views

    Watu wengi huogopa sio Tu kumkaribia nyoka Bali pia kumtazama tu. Hata hivyo Kwa Rukiya Mohamed kutangamana na nyoka imekuwa kama sehemu ya maisha yake. Afisa huyo wa shirika la KWS ni kiungo muhimu katika harakati za shirika Hilo za kudhibiti mzozo baina ya wanyama pori na binadamu, huku akiwa mwanamke WA pekee anayehudumu katika kitengo cha kudhibiti nyoka kwenye ukanda WA Pwani. Nilipata fursa ya kukutana naye akiwa kwenye pilkapilka za kazi yake na hii Leo ndiye tunayemvisha Taji la mwanamke Bomba.