Mwanamke Bomba | Safari ya Alice Muhonja baada ya mchafuko wa uchaguzi wa 2007

  • | Citizen TV
    1,033 views

    Mbali na kusababisha maafa na wengi kupoteza makao , Machafuko ya baada ya uchaguzi wa mwaka 2007 yaliathiri maisha ya watu wengi Kwa kiwango kikubwa. Hata hivyo Kwa Alice Muhonja ilikuwa mwanzo WA safari ambayo imebadilisha sio Tu maisha yake Bali pia ya watu wengi katika Mtaa wa molem eneo la komarock. Alianza Kwa kuwapa hifadhi watoto waliokuwa wakihangaika kufuatia ghasia za baada ya uchaguzi na sasa amefanikiwa kufungua shule ambayo inasomesha bila malipo watoto wanaotoka familia zisizojiweza huku kina mama wakifaidika kupitia miradi aliyoanzisha chini ya shirika la safisha Afrika.