Mwanamme amuua mkewe kisha kujiua eneo la Mwingi

  • | Citizen TV
    296 views

    Familia moja kutoka wadi ya MUI Kaunti Ndogo ya mwingi east inaomboleza vifo vya mwanamke na mumewe. Hii ni baada ya mume huyo kumuua mkewe kwa kumkatakata kwa panga na kisha kujitoa uhai kwa kunywa sumu. Inaarifiwa kuwa wawili hao walikuwa wanazozana mara kwa mara. Aidha, inadaiwa kuwa hii si mara ya kwanza kwa mume huyo kuhusika na ugomvu na mkewe na wakaazi wanaripoti kuwa polisi waliwahi kuingilia kati mzozo huu. Polisi wanasema wameanzisha uchunguzi kuhusiana na mauaji haya