Mwanamume adaiwa kumnajisi binti ya mpenziwe eneo la Narok

  • | Citizen TV
    682 views

    Mwanamme mmoja anadaiwa kumvamia binti ya mpenziwe na kumdhulumu kimapenzi katika kaunti ya Narok. Kwa sasa mshukiwa huyo amekamatwa na ataendelea kuzuiliwa huku msichana huyo wa miaka kumi akipokea matibabu na ushauri nasaha. Tukio hili la kutamausha lilitokea katika eneo la kibiashara la Nairegie Enkare, eneo bunge la Narok mashariki mtaa wa Soweto. Mtoto huyo amesimulia kilichojiri ijumaa huku akieleza kuwa mwanamume huyo alimnyemelea alipokuwa akiosha viombo. Mamake mzazi anakiri mshukiwa mwenye umri wa miaka 41 ni mpenziwe ambaye alikosana na mkewe kabla ya kuanza kuishi naye.