Mwanamume amuua msichana eneo la Kiambaa

  • | KBC Video
    45 views

    Maafisa wa polisi katika eneo la Kiambaa kaunti ya Kiambu, wanamzuilia mshukiwa mmoja anayedauwa kumuua mtoto wa miaka minane. Akithibitisha kisa hicho, Kamanda wa polisi eneo la Kiambaa, Pius Mwanthi alisema jaribio la mshukiwa huyo la kutoroka liligonga mwamba pale alipoanguka kwenye shimo karibu na karibu na nyumba alikotekeleza mauaji hao na kuokolewa na maafisa wa polisi kwa ushirikiano na wazimamoto. Mwanthi alisema mshukiwa huyo alijaribu kumuua mamake mtoto huyo lakini hakufaulu baada ya mama huyo kutoroka. Wakaazi wa eneo hilo wamelaani kitendo hicho wakitaka mshukiwa achukuliwe hatua kali za sheria.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive