Mwanamume kutoka kaunti ya Baringo amuua mkewe kwa kumdunga mkuki

  • | Citizen TV
    391 views

    Mwanamume mmoja katika kijiji cha Kibonjos eneo la Kiptagich kaunti ya Baringo anadaiwa kumuua mkewe kwa kutumia mkuki uliokuwa na sumu. Kulingana na majirani, wawili hao wamekuwa wakipigana mara kwa mara. Mwanamume huyo anadaiwa kumdunga mkewe kwa mkuki baada ya kubugia pombe haramu inayouzwa hatua chache kutoka nyumbani kwa kamishna msaidizi na chifu wa eneo hilo. Wakazi wanawalaumu maafisa hao wawili kwa kufumbia macho uuzaji wa pombe hiyo haramu eneo hilo.