Mwanaume akamatwa na watu wanaoaminika kuwa polisi Garissa

  • | Citizen TV
    1,244 views

    Familia moja katika kijiji cha Bula Mzuri kaunti ya Garissa ina wasiwasi mkubwa wasijue aliko jamaa yao Mohammed Ahmed Nur aliyetekwa nyara usiku wa kuamkia jana na watu wanaoaminika kuwa maafisa wa usalama. Kulingana na walioshuhudia tukio hilo, watu hao walijaribu kufungua mlango wa nje wa nyumba alimokuwa Mohamed kwa nguvu na waliposhindwa waliruka ukuta na kuingia katika boma hilo. Watu hao kisha walimkamata mtu huyo na kutoweka naye kwa kutumia gari aina ya Land Cruiser. Familia ya jamaa huyo sasa inataka vitengo vya usalama kumwasilisha mahakamani iwapo alivunja sheria badala ya kumpeleka mahali isiyojulikana. Kwa upande wao Polisi wanasema familia imeandikisha taarifa na kwamba uchunguzi utafanywa kutegua kitendawili hicho.