Mwanaume atiwa mbaroni kwa kuficha mwili wa mamake nyumbani

  • | K24 Video
    463 views

    Mwanamume wa umri wa miaka 45 katika kaunti ya Kirinyaga ametiwa mbaroni na maafisa wa polisi kwa kuuficha mwili wa mamake nyumbani kwake akitumaini kuwa atafufuka baada ya maombi. Kulingana na familia, mwanamume huyo, James Njiine alimtoa mamake hospitali alipokuwa akiuguzwa na kumpeleka nyumbani kwake kumfanyia maombi kwani madhehebu yake hairuhusu matibabu ya hospitali.