Mwandamanaji aliyejeruhiwa Jumanne atolewa risasi saba

  • | Citizen TV
    3,198 views

    Samuel Omondi Okoth mwenye umri wa miaka 21 ana matumaini ya kutembea tena baada ya kuponea chupuchupu wakati wa maandamano ya Jumanne. Alipigwa risasi nane za mpira mgongoni, ambapo madaktari katika Hospitali ya Kitaifa ya Kenyatta wamefaulu kuondoa risasi saba. Ya mwisho, ambayo bado imejikita karibu na uti wa mgongo,inatishia uwezo wake wa kutembea na ndiyo sababu haikuondolewa. Ode Francis alimtembelea hospitalini na kuandaa taarifa ifuatayo.