Mwangi Wa Iria atakiwa afike EACC kabla ya kufikishwa mahakamani

  • | K24 Video
    157 views

    Mahakama kuu sasa imeondoa agizo la kuzuia kukamatwa na kushtwakiwa kwa aliyekuwa Gavana wa Murang'a Mwangi Wa Iria, mkewe pamoja na washukiwa wengine sita huku wakitarajiwa mahakamani hapo kesho.wa iria na wenzake watashtakiwa kwa madai ya sakata ya milioni mia moja arobaini ya utoaji zabuni alipohudumu kama gavana wa Murang'a. Vilevile afisa mkuu mtendaji wa Bomas of Kenya anayeandamwa na kesi ya ufisadi ameachiliwa kwa dhamana shilingi milioni moja pesa taslimu au bondi ya milioni tano.