Mwenyekiti mteule wa IEBC ajitetea mbele ya kamati ya bunge

  • | Citizen TV
    1,132 views

    Shughuli ya kumpiga msasa mwenyekiti mteule wa IEBC Erastus Ethekon na makamishna wateule ilifanyika leo huku kamati ya masuala ya sheria ya bunge la kitaifa ikizua masuali kuhusu uhusiano kati ya walioteuliwa na maafisa wakuu serikalini. Mwenyekiti mteule Ethekon amekanusha madai ya kuwa na uhusiano wa karibu na naibu msimamizi wa ikulu Josphat Nanok. Kwa upande wake Hassan Noor Hassan aliyeteuliwa kuwa kamishna amekiri kwamba ana uhusiano na kiongozi wa wachache katika bunge la kitaifa Junet Mohamed.