- 259 viewsDuration: 1:41Mwezi wa Aprili huwa mwezi wa uhamasishaji kuhusu hali ya tawahudi duniani. kuhitimisha kampeni ya mwaka huu, walezi kwa ushirikiano na wadau wa afya walifanya matembezi ya kilomita 50 kutoka Nairobi hadi Thika. Matembezi hayo yalianza katika mzunguko wa Roysambu, yakilenga kutoa ujumbe kuhusu umuhimu wa malezi na msaada sahihi kwa watoto wenye tawahudi. Wadau wamewataka wakenya kupinga unyanyapaa na ubaguzi dhidi ya watoto wenye tawahudi.