Mwili wa mchimba mgodi aliyekuwa akitafutwa wapatikana

  • | Citizen TV
    1,502 views

    Hatimaye mwili wa mchimba mgodi wa dhahabu uliokuwa ukitafutwa kwa zaidi ya wiki moja sasa eneo la sigalagala eneo bunge la ikolomani umeondolewa. kupatikana kwa mwili huo kumefanya idadi ya waliofariki baada ya timbo kuporomoka kuwa watu wanne. Waokoaji kutoka kaunti za nyanza na kakamega walishirikiana kuupata mwili huo ambao ulikuwa tayari umeoza. serikali ya kaunti ya kakamega imeraiwa kutafuta huduma za waokoaji hapo kunapotokea janga kwani wana ujuzi wa kutosha. Aidha mashirika yanayoangazia usalama wa migodi nchini yameonya wachimbaji migodi dhidi ya kuendeleza shughuli zao bila magwanda ya kujikinga.