Mzimbabwe anayeishi nchini Israeli anasema hali ni tete Tel Aviv⁣ ⁣

  • | VOA Swahili
    642 views
    Kilichotokea tuliamka jana asubuhi na kusikia ving’ora. Hiyo ni kwa sababu tulikuwa tunashambuliwa huku roketi zikifyatuliwa kutoka Gaza. Ilikuwa ni Jumamosi ya kawaida, kama ilivyo siku yoyote ya Sabato.⁣ Watu hapa hupumzika siku ya Sabato. Kwa hiyo kuamka tu jana na kusikia ving’ora na boom, boom. Milio ya mfumo wa ulinzi wa anga wa Iron Dome ukizuia roketi.⁣ Basi kilichotokea ni Hamas, ambayo ni taasisi ya kigaidi yenye makao yake Gaza, ambayo siku zote inapigana na Israeli, iliamua kulishtukiza Jeshi la Ulinzi la Israeli jana asubuhi.⁣ Hili halijawahi kutokea. Kwa kawaida wanachofanya huwa wanafyatua roketi kutoka upande huo. Lakini walichofanya leo, jana, siyo tu walifyatua roketi, lakini na amini walifyatua roketi baada ya wao kuwa tayari ndani ya Israeli…⁣ ⁣⁣ #israel #gaza #reels #igreels #videography #voa #hamas #mzimbabwe #telaviv #tete #israeli