- 523 viewsDuration: 3:38Mzozo mkali wa ardhi umeubuka katika mpaka wa Kaunti za Laikipia na Samburu. Gavana wa Samburu Jonathan Lati alitangaza kuwa ardhi ya Kirimon eneo la Laikipia Kaskazini yenye ekari elfu 44 inapaswa kugawiwa jamii ya Wasamburu. Ni kauli ambayo imezua mjadala mkali na hisia mseto miongoni mwa viongozi wa kaunti ya Laikipia, ambao sasa wanamtuhumu Gavana huyo kwa kuingilia masuala ya kiutawala ya kaunti jirani.