Mzozo wa ardhi I Maelfu ya familia Msambweni kulala kwenye kibaridi baada ya nyumba zao kubomolewa

  • | KBC Video
    51 views

    Maelfu ya familia hukoMsambweni eneo bunge la Voi katika kaunti ya Taita Taveta huenda zikalala kwenye kibaridi baada ya nyumba zao kubomolewa na mjenzi wa kibinafsi. Mjenzi huyo wa kibinafsi anadai kumiliki ardhi ambako familia hizo zimeishi kwa miaka mingi. Familia zilizoathirika zimesema hazikupewa ilani yoyote ya kuwafurusha kabla ya ubomoaji huo. Baadhi yao walikuwa wameenda kazini huku wengine wakiamshwa na kamsa za majirani zao kwenye kisa hicho kilichotokea mapema asubuhi.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive