Mzozo wa ardhi ya cheluget huko Narok watokota

  • | Citizen TV
    1,395 views

    Mvutano mpya umeibuka kuhusu shamba la ekari 5,800 la familia ya marehemu isaiah cheluget, ambalo rais william ruto alisema serikali itanunua na kuwahamishia wakimbizi wa mau. Mwanawe mmiliki wa ardhi hiyo, moses kipkirui cheluget, alipinga kauli hiyo na kutishia kwenda mahakamani kuzuia mpango huo. Hata hivyo, jumamosi hii, upande mwingine wa familia ukiongozwa na balozi wa zamani nancy kirui cheluget, ulithibitisha kuendelea na mazungumzo na serikali na kumtaja kipkirui kuwa si mmoja wao.