Mzozo wa steni Kisumu kati ya wahudumu wa magari ya umma na serikali ya kaunti

  • | Citizen TV
    979 views

    Kizaazaa kimeripotiwa kaunti ya Kisumu, ambako wahudumu wa magari ya umma wamekaidi agizo la kaunti kuwataka kuhama hadi kwenye steni ya Kisumu. Ilani hiyo iliyochapishwa Jumamosi na usimamizi wa jiji la Kisumu, iliagiza kuwa magari yote yanayoegeshwa kando ya barabara kuu ya Kisumu kuelekea Nairobi yatafute sehemu ndani ya steni ya Kisumu kuanzia leo Jumatatu, la sivyo magari hayo yatazuiliwa.