Mzozo wa uongozi wa SUPKEM watokota

  • | Citizen TV
    706 views

    Mzozo wa uongozi katika baraza kuu la waislamu nchini SUPKEM umeendelea huku sasa mrengo unaoongozwa na aliyekuwa mwenyekiti Yusuf Nzibo kuzuiwa kuingia katika afisi za baraza hilo. Hii ni licha ya amri ya mahakama iliyozuia maafisa wa sasa wakiongozwa na Hassan Ole Nado kuendesha shughuli zozote kwa niaba ya SUPKEM.