Naibu gavana wa Homa Bay Joseph Magwanga anasema amepokea vitisho

  • | Citizen TV
    954 views

    Naibu gavana wa kaunti ya Homa Bay Joseph Oyugi Magwanga anasema maisha yake yako hatarini. Mangwanga anadai kupokea vitisho kabla ya watu wasiojulikana kuvamia nyumba yake huko Oyugi's Homa Bay jana usiku. Magwanga anasema kuwa walinzi wake walifyatuliana risasi na watu hao. anasema kuwa alilazimika kubadilisha magari alipoarifiwa kuwa watu wasiojulikana walionekana nje ya nyumba yake. watu hao wanadaiwa kuvamia gari la Magwanga wakidhania alikuwa ndani.