Naibu rais akanusha kuhusika na sakata ya ulaghai inayomhusu Rashid Echesa

  • | Citizen TV
    Kinara wa ODM Raila Odinga na kiongozi wa wachache katika seneti James Orengo wanamtaka naibu wa Rais William Ruto kuweka bayana anayoyafahamu kuhusu tuhuma za utapeli zinazomkabili aliyekuwa waziri wa michezo Rashid Echesa. Wawili hao wanadai kuwa ofisi ya naibu wa rais katika jumba la Harambee Annex ilitumika kama eneo la mikutano kati ya Echesa na wawekezaji waliopokezwa stakabadhi ghushi za zabuni. Na kama anavyotuarifu francis gachuri, ruto amejitenga na madai hayo na kudai wapinzani wake wanajaribu kumpaka tope.