Naibu Rais Gachagua asema hakuna mgawanyiko Mlima Kenya

  • | Citizen TV
    1,375 views

    Naibu rais Rigathi Gachagua ameendelea kushikilia kuwa hakuna mgawanyiko wa viongozi katika eneo la kati. Gachagua akieleza kuwa viongozi wa eneo la kati huenda wakatofautiana katika misimamo yao ya kisiasa ila umoja wao kama viongozi wa eneo moja unasalia. Aidha, naibu rais ameahidi kukabiliana na walaghai katika sekta ya kahawa eneo hilo. Amezungumza haya akiwa kaunti ya Nyeri ambako ameoongoza shughuli ya kuchangisha pesa za kujenga kanisa la PCEA Kagere eneobunge la Othaya