Naibu rais Gachagua azindua mfumo wa kidijitali wa usimamizi wa safari za nje za maafisa wa serikali

  • | Citizen TV
    479 views

    Serikali imezindua mfumo wa kidijitali wa usimamizi wa safari za nje za maafisa wa serikali. Hii ni katika juhudi za kuhakikisha usafiri unaowahusisha mawaziri na maafisa wengine wakuu wengine serikalini unadhibitiwa na kupigwa darubini na afisi ya utumishi wa umma. Naibu rais Rigathi Gachagua akizungumza kwenye hafla hii amesema kuwa mfumo huo utapunguza utumizi mbaya wa pesa za umma.