Naibu rais Kindiki asema wako tayari kupoteza umaarufu

  • | Citizen TV
    2,076 views

    Naibu rais Kithure Kindiki sasa anasema ni heri kwa serikali kupoteza umaarufu wake kuliko kupoteza mwelekeo wa taifa. Kindiki aliyewaongoza viongozi wanaoegemea kenya kwanza kwa Zoezi la uwezeshaji katika maeneo bunge ya Kathiani na mwingi ya kati, pia amewazomea viongozi wa upinzani na mabalozi wa nchi za kigeni wanaoonekana kushabikia maandamano yanayoendelezwa na vijana. Ameendelea kuonya kwamba serikali haitorusu matukio ya hivi majuzi kushuhudiwa tena.