Naibu Rais Rigathi Gachagua afanyiwa maombi Meru, akiomba kupewa muda zaidi

  • | Citizen TV
    14,176 views

    Naibu Rais Rigathi Gachagua aligeukia maombi leo, baada ya joto la siasa la kutaka atimuliwe afisini kupanda hata zaidi. Gachagua aliyehudhuria ibada kaunti ya meru akiwataka wabunge wanaomchongea kuheshimu uamuzi wa wakenya wa kumchagua yeye kama naibu rais. Na kama anavyoarifu Emmanuel Too, Spika wa Bunge la taifa Moses Wetang’ula ameongoza wabunge wanaompinga Gachagua kuunga mkono hoja ya ya kumpiga kalamu kama naibu rais.