Naibu rais Rigathi Gachagua akosa kuafikiana na magavana kuhusu fedha za kaunti

  • | K24 Video
    100 views

    Kikao cha baraza la bajeti na uchumi (IBEC) baina ya naibu rais Rigathi Gachagua na magavana hii leo kimeshuhudia vuta ni kuvute kikikosa kuafikiana kuhusu mgao wa fedha kwa kaunti. Sasa rais William Ruto atalazimika kufanya mkutano mwingine wa siku mbili mapema mwezi ujao naivasha ili kukwamua kitendwaili, cha kaunti zitengewe kiasi gani katika mwaka wa kifedha unaokuja.