Naibu rais William Ruto aongoza kampeni katika kaunti ya Narok na Kiambu

  • | K24 Video
    28 views

    Naibu rais William Ruto amewataka wakaazi wa kaunti ya Narok kutowachagua viongozi wasiokuwa na miradi ya kuonyesha utendakazi wao. Akizungumza katika kaunti za Narok na Kiambu alikoongoza kampeni zake, Ruto amesema atawashika mikono viongozi watakaochaguliwa chini ya chama cha UDA na kuhakikisha wanachapa kazi bila kubagua wengine. Hata hivyo katika mkutano wa Kiambu, wagombea ugavana ambao wako katika muungano wa Kenya Kwanza, wakiwa pamoja na William Kabogo wa chama cha tujibebe na Moses Kuria wa Chama Cha Kazi hawakuhudhuria.