Naibu wa rais Rigathi Gachagua awatia moyo watahiniwa Komarock

  • | Citizen TV
    352 views

    Naibu wa rais Rigathi Gachagua alikuwa katika shule ya msingi ya Komaroc katika eneobunge la Embakasi Central hapa jijini Nairobi katika siku ya pili ya mtihani wa KCPE na KPSEA. Rigathi amewaambia watahiniwa kuwa alifika shuleni humo mapema kuwatia moyo pamoja na kuwasilisha ujumbe wa rais kwao. Kulingana na Rigathi, serikali imejizatiti kuboresha mfumo wa elimu na kwamba rais atapokea ripoti ya kwanza wa jopokazi la kurekebisha mfumo wa elimu Ijumaa hii