Naivas wabanwa na Nairobi United kwenye mechi ya ligi ya Super

  • | Citizen TV
    136 views

    Vinara wa supa ligi Naivas FC walilazimishwa sare ya bao moja na Nairobi United asubuhi ya leo. Nairobi waliokuwa nyumbani uwanjani Mpesa mjini Thika walitangulia kwa bao la dakika ya 33 kupitia kwa Rodgers Angal bao lililodumu hadi kipindi cha kwanza. Wanamaduka wa Naivas walirudi na kusawazisha kupitia kwa Robert Karisa dakika ya 71. Naivas wangali kileleni kwa alama 58, alama moja zaidi ya Mathare walioshinda mbili moja dhidi ya Mombasa Elite.